Shirika la Tor Project, Inc, lilianzishwa kama shirika lisilo la faida la 501(c)(3) mwaka wa 2006, lakini wazo la "onion routing" lilianzia katikati ya miaka ya 1990.

Kama watumiaji wa Tor, waendelezaji, watafiti, na waanzilishi ambao wamewezesha Tor ni kundi la watu wenye utofauti. Lakini watu wote ambao wamehusika na Tor wameungana na imani moja: watumiaji wa mtandao wanapaswa kuwa na ufikiaji wa faragha kwenye tovuti isiyodhibitiwa.

Katika miaka ya 1990, ukosefu wa usalama kwenye mtandao na uwezo wake wa kutumiwa kwa ajili ya kufuatilia na uchunguzi ulikuwa wazi, na mwaka 1995, David Goldschlag, Mike Reed, na Paul Syverson kutoka Kituo cha Utafiti cha Majini cha Marekani (NRL) walijiuliza iwapo kuna njia ya kuunda uhusiano wa mtandao ambao hauonyeshi ni nani anayezungumza na nani, hata kwa mtu anayechunguza mtandao. Jibu lao lilikuwa ni kuunda na kuweka kwenye matumizi ya kwanza miundo na vielelezo vya utafiti wa kutelezesha onion.

Malengo ya Onion routing ilikuwa kuwa na njia ya kutumia mtandao wa intaneti kwa faragha iwezekanavyo, na wazo lilikuwa kuelekeza usafirishaji wa data kupitia seva nyingi na kuisimbua kila hatua. Haya bado ni maelezo rahisi juu ya jinsi Tor inavyofanya kazi sasa.

mwanzoni mwa miaka ya 2000, Roger Dingledine, aliyehitimu hivi karibuni kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Massachuse (MIT) alianza kufanya kazi kwenye mradi wa onion routing wa NRL pamoja na Paul Syverson. Kuweza kutofautisha kazi halisi kutoka kwa juhudi nyingine za onion routing zilizokuwa zinaanza kujitokeza mahali pengine, Roger aliita mradi huo Tor, ambayo ilimaanisha The Onion Routing. Nick Mathewson, mwanafunzi mwenzake wa Roger katika Chuo Kikuu cha MIT, alijiunga na mradi huo haraka baada ya hapo.

Tangu kuanzishwa kwake katika miaka ya 1990, onion ilianzishwa ili kuzingatia mtandao usio na kituo kimoja. Mtandao ulihitajika kuendeshwa na taasisi zenye maslahi na matarajio tofauti ya uaminifu, na programu ilihitajika kuwa huru na wazi ili kuongeza uwazi na usambazaji usio na kituo kimoja. ndio maana mwezi Oktoba 2002, mtandao wa Tor ulipotumiwa kwa mara ya kwanza, na ndipo kanuni zake zilipotolewa kwa leseni ya programu huria na wazi. kufikia mwisho wa 2003, mtandao ulikuwa na watu wengi wanaojitolea, hasa U.S., ukiongeza nyingine na ujerumani.

Kutambua faida za Tor kwa haki za kidijitali, shirika la Electronic Frontier Foundation (EFF ilianza kufadhili kazi ya Roger na Nick kuhusu Tor mwaka 2004. Mwaka 2006, Tor project , Inc., shirika lisilokuwa la kibiashara lenye namba ya usajili 501(c)(3), lilianzishwa ili kusimamia maendeleo ya Tor.

Mwaka wa 2007, shirika liliendeleza viungio kwenye mtandao wa Tor ili kukabiliana na ukandamizaji wa kimaandishi, kama vile uhitaji wa kupita kwenye vifaa vya ulinzi vya kiserikali, ili watumiaji wake waweze kupata mtandao wazi.

Tor ilianza kupata umaarufu miongoni mwa wanaharakati na watumiaji wenye uelewa wa teknolojia waliopenda faragha, lakini ilikuwa ngumu kwa watu wasio na ujuzi wa kiteknolojia kuutumia. Kwa hiyo, kuanzia mwaka wa 2005, maendeleo ya zana zaidi ya zile za mtandao wa Tor yalianza ili kufikia watumiaji wenye ujuzi mdogo wa kiteknolojia. maendeleo ya Tor Browser yalianza mwaka 2008.

Kwa kuwa Tor Browser imefanya Tor iweze kupatikana zaidi kwa watumiaji wa kawaida wa mtandao na wanaharakati, Tor ilikuwa kifaa muhimu wakati wa Mapinduzi ya Kiarabu Arab Spring yaliyoanza mwishoni mwa mwaka 2010. Haikulinda tu utambulisho wa watu mtandaoni, lakini pia iliwawezesha kupata rasilimali muhimu, mitandao ya kijamii, na tovuti ambazo zilikuwa zimefungwa.

Mahitaji ya zana za kuhakikisha ulinzi dhidi ya upelelezi mkubwa yalikuwa suala kuu la umma baada ya ufunuo wa Snowden mwaka 2013. Sio tu ilikua kwa chombo cha Tor kwa sehemu ya whistleblowing, lakini dhamira za hati pia huzingatia uhakika huo, kwa muda, Tor haiwezi kuharibika.

Ufahamu wa watu kuhusu ufuatiliaji, uchunguzi, na udhibiti wa mtandao unaweza kuwa umeongezeka, lakini pia idadi ya vikwazo hivi kwa uhuru wa mtandao imeongezeka. Leo hii, mtandao wa Tor maelfu ya relays zinazoendeshwa na wanaojitolea na watumiaji milioni kote duniani. Na ni aina hii ya utofauti ambao unawawezesha watumiaji wa Tor kuwa salama.

Sisi, Tor project, tunapambana kila siku ili kila mtu awe na ufikiaji wa faragha kwenye mtandao usiodhibitiwa, na Tor imekuwa zana yenye nguvu zaidi duniani kwa ajili ya faragha na uhuru mtandaoni.

Lakini Tor ni zaidi ya programu tu. Ni kazi ya upendo iliyoanzishwa na jamii ya kimataifa ya watu waliojitolea kwa haki za binadamu. Tor project imejitolea sana kwa uwazi na usalama wa watumiaji wake.